Connect with us

Soka

Caf Yaipa Shavu Simba sc

Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) imeiruhusu klabu ya Simba sc kuingiza mashabiki elfu 35 katika mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho dhidi ya Asec Mimosas siku ya tarehe 13 mwezi huu mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na michezo iliyopita ambapo hivi sasa Caf imekua na utaratibu wa kuruhusu mashabiki wachache kutokana na kuwepo kwa janga la ugonjwa wa uviko 19 hivyo kuzuia idadi kubwa ya mashabiki ni njia mojawapo ya kudhibiti usambaaji wa ugonjwa huo.

Mwezi huu wa Februari klabu hiyo itakua na vibarua vigumu katika michezo miwili ya ndani dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya Kwanza huku ikivaana na Asec Mimosas,USGN na Rs Berkane ndani ya wiki mbili katika kombe la shirikisho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka