Connect with us

Soka

Bruce afutwa kazi Newcastle United

Uongozi wa klabu ya soka ya Newcastle United ya Uingereza umemfukuza akocha mkuu wa timu hiyo Steve muda mchache uliopita mara baada ya mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye ligi kuu soka nchini Uingereza.

Uamuzi huo ulikuwa ni jambo la muda tu baada ya klabu hiyo kununuliwa na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohamed Bin Sakman.

Kwasasa timu hiyo inasaka kocha mkuu mpya huku kocha wa zamani wa AS Roma Mreno Paul Fonseca akitajwa zaidi kuwa huenda akachukua mikoba hiyo ya kuifundisha Newcastle.

Makocha wengine wanaotajwa kwenye orodha hiyo ni kocha wa Rangers Steven Gerard,Brendan Rodgers,kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Lucien Favre na kocha wa Brighton and Hove Albion Graham Potter.

Newcastle United ipo kwenye mikakati mizito ya kuboresha idara mbalimbali ndani ya timu kuanzia benchi la ufundi,idara ya usajili na utawala ili kuwa moja ya klabu kubwa nchini humo na duniani kwa ujumla.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka