Connect with us

Soka

Bilionea wa Czech aongeza nguvu West Ham United

Bilionea kutoka Jmahuri ya watu wa Czech Daniel Kretinsky amekamilisha mchamkato wa manunuzi ya hisa ndani ya klabu hiyo kwa kuchukua takribani 27% ya hisa zote za timu hiyo.

Kretinsky ambaye ni mfanyabiashara na mwanasheria kitaaluma ataungano na wenyeviti wenza David Sullivan na David Gold pamoja na makamu mwenyekiti Karen Brady katika bodi ya timu hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari makamu mwenyekiti Karen Brady amesema ”ninayo furaha kumkaribisha Daniel Kretinsky,Pavel Horsky pamoja na 1890s holdings a.s ndani ya West Ham,siku zote tumekuwa tukiangalia kusonga mbela hivyo uwekezaji wa Daniel ni ufunguo muhimu katika kuleta maendeleo ndani ya klabu na kukuza nafasi ya klabu yetu”.

”Uzoefu wake mkubwa katika masuala ya biashara na ulimwengu wa soka utainufaisha sana klabu.

West Ham imeanza vizuri ligi kuu ya Uingereza kwa kushika nafasi ya nne hadi sasa huku wakifanikiwa kusonga mbele katika hatua ya mtoano ya kombe la Europa pamoja na robo fainali ya kombe la ligi,na uwekezaji wa Daniel ni dalili za msimu mzuri kwa klabu hiyo.

Muwekezaji huyo pia anaimilika klabu kubwa ya Sparta Praha ya huko Czech na uwepo wa wachezaji kutoka nchi hiyo Tomas Soucek na Coufal umeongeza mashabiki wa klabu hiyo nchini humo hali ilyomfanya aone ni fursa kibiashara.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka