Connect with us

Soka

Bilionea Mganda Kuinunua Chelsea

Joel Jaffer A’ita amekuwa gumzo baada ya kuwasilisha ombi la kuinunua Klabu ya Soka ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza ambayo imewekwa sokoni na Tajiri Roman Abramovich kutokana na sababu za kisiasa.
Mhandisi huyo wa Ujenzi ambaye ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, pia anamiliki Klabu ya Michezo ya Arua Hill ya Ligi Kuu ya Uganda ambapo aliwasilisha rasmi ombi lake la kuinoa The Blues, na kuwa raia wa pili wa Uganda kutoa zabuni kwa klabu ya soka ya Uingereza baada ya jaribio la Michael Ezra Mulyoowa kwa Leeds United mwaka 2004 (Pauni Milioni 60).
“Niko tayari kutwaa Klabu ya Soka ya Chelsea ” A’ita aliiambia Kawowo Sports Media Alhamisi, Machi 3, 2022. A’ita anatoa ofa ya dola bilioni 3.3 kwa Bilionea wa Urusi Roman Abramovich, mmiliki wa Klabu ya Soka ya Chelsea na anakusudia kuuita klabu hiyo Klabu ya Soka ya Kongolo (Kongolo FC).
“Kufuatia taarifa kwa umma kuhusu nia ya kuuza Chelsea FC, ningependa kueleza nia yetu ya kununua klabu. Kwa thamani ya sasa ya $ 3.2 bilioni, tunatoa $ 3.3 bilioni. Tunakusudia kubadili jina la klabu kama Kongolo FC” Aita aliandika barua kwa Abramovich.
Aita aliingia katika ulingo wa soka nchini Uganda mwaka wa 2019 alipotwaa Klabu ya Soka ya Doves All Stars.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka