Connect with us

Soka

Biashara Utd yafanya biashara nzuri kwa Mkapa

Wanajeshi wa mpakani Biashara United ya Mara imeanza vema mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Al Ahly Tripoli kwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 nyumbani kwa Mkapa katika hatua ya awali kufuzu makundi kombe la shirikisho barani Afrika.

Biashara wanaotumia uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam kama uwanja wao wa nyumbani kwenye michuano hiyo walijipatia goli la uongozi dakika ya 39 kupitia kwa Deogratius Mafie,Wanajeshi hao walijipatia goli la pili kunako dakika ya 60 kupitia kwa mshambuliaji Atupele Green kwa mkwaju mkali  nje ya kumi na nae.

Ushindi huo ni mtaji mzuri kwa Biashara Utd kuelekea mchezo wa marudiano mjini Tripoli Libya ndani ya wiki moja.

Wawakilishi wengine wa Tanzania kwenye michuano hiyo Azam Fc wao watashuka dimbani hapo kesho kwenye mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Mafarao Pyramids wa Misri kwenye dimba la Chamazi saa tisa alasiri.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka