Connect with us

Soka

Benchika Arejea Simba sc

Kocha mkuu wa klabu ya Simba sc Abdelhack Benchika amerejea katika klabu hiyo baada ya kukosekana kwa siku kadhaa kufuatia kuhudhuria mafunzo maalumu ya ukocha nchini kwao Algeria na kuikosa baadhi ya michezo ya ligi kuu ya Nbc ambayo timu hiyo ilicheza.

Taarifa ya awali iliyotolewa na klabu hiyo ilisema kuwa kocha huyo angekosekana katika michezo dhidi ya Coastal Union na Singida Fountain Gate ambayo yote miwili timu hiyo iliibuka na ushindi na kuzoa jumla ya alama sita na sasa taarifa zinasema kuwa kocha huyo amerudi na ataongoza mazoezi ya timu hiyo jioni ya leo na kesho atakuwepo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc March 15.

Katika michezo miwli iliyopita Simba sc ilisimamiwa na wasaidizi wa Benchika aliokuja nao kutoka nchini Algeria wakati anafika ambao walisaidiana na Selemani Matola kuongoza jahazi hilo.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu nchini Simba sc ipo nafasi ya tatu ya msimamo ikiwa na alama 42 baada ya kucheza michezo 18 huku Yanga sc ikiwa kileleni na alama 49 katika michezo hiyo hiyo 18 ya ligi kuu na nafasi ya pili ipo Azam Fc yenye alama 44 ikiwa imecheza michezo 20 ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka