Connect with us

Soka

Benchika Akalia Kuti Kavu Simba sc

Baadhi ya mabosi wa klabu ya Simba sc wameanza kumtolea macho kocha Abdelhack Benchika kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu ambapo timu hiyo imecheza jumla ya michezo mitano mfululizo bila kupata ushindi.
Mabosi hao wameanza kuwa na wasiwasi na mbinu za kocha huyo pamoja na uchaguzi wa kikosi kutokana na kukosa ushindi huku wakikubali kipigo cha pili mfululizo kutoka kwa Yanga sc ambao ni watani wao wa jadi.
Kitendo cha kocha huyo kumuweka benchi Luis Miqquison ambaye amekua akiipa uhai timu hiyo mara anapoingia kikosini kumewafanya pia mabosi hao kuanza kumtilia mashaka huku kauli yake ya kutaka mastaa wa nguvu kikosini humo ambapo mwisho mwa msimu zaidi ya mastaa nane watatemwa kikosini humo.
Benchika mara baada ya mchezo wa Yanga sc alisema kuwa haridishwi na viwango vya mastaa wengi kikosini humo hivyo kuhitaji wapya msimu ukiisha “Tangu nimeanza kufundisha mpira sikuwai kukutana na timu yenye wachezaji wagumu kuelewa kama hii simba timu inacheza tofauti kabisa na matakwa yangu”. Alisema kocha huyo kwa uchungu

“Nitaongea tena na viongozi wangu kama nitakubaliwa kuunda timu yangu upya msimu ujao ili niandae list yangu ya wachezaji nitakaoweza kuunda timu bora Africa ila kama watashindwa kukubaliana na mimi basi watambue kuwa CV yangu sijaitengeza na pesa nashuka CV yangu kila kukicha naweza kufanya maamuzi sahihi”Alisema Benchika
Ripoti kutoka nchini kwao Algeria zinasema kuwa kocha huyo anahitajika na vilabu vya Cr Belouzdad,Wydad Ac na timu za nchini Misri nazo zinamtolea macho huku taarifa zikidai kuwa hana maisha marefu klabuni Simba sc kutokana na kutofautiana na viongozi kwenye baadhi ya mambo ya usajili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka