Connect with us

Soka

Basena Atimuliwa Ihefu Fc

Klabu ya Ihefu Fc imeachana na kocha raia wa Uganda Moses Basena kutokana na kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya klabuni hapo tangu ajiunge nayo akichukua nafasi ya Zubeiry Katwila aliachana na timu hiyo na kujiunga na Mtibwa Sugar.

Basena amedumu kikosini humo kwa siku hamsini pekee huku akipata sare na vipigo pekee katika michezo saba ya ligi kuu tangu ajiunge na klabu hiyo.

Licha ya kuwa na mastaa wengi kikosini humo Basena ameshindwa kuwatumia mastaa hao ili wampe matokeo ya ushindi ambapo mastaa kama Fikirini Bakari,Juma Nyoso,Victor Akpan na wengineo.

Basena anaungana na makocha wengine kama Roberto Oliveira “Robertinho” wa Simba sc,Zubeiry Katwila,Hans Van Pluijm wa Singida Fountain Gate,Melis Medo wa Dodoma Jiji pamoja na wengine ambao kwa muda tofauti msimu huu wameachana na timu zao kwa sababu mbalimbali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka