Connect with us

Soka

Bajana,Ndoye Kutibiwa Afrika Kusini

Klabu ya Azam Fc imetangaza kuwa mastaa wake wawili Sospeter Bajana na Malickou Ndoye wataondoka kwenda nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya matibabu ya nyonga katika hospitali ya Vicent Palloti iliyopo jijini Cape Town nchini humo.

Mastaa hao walimia kwa nykati tofauti tofauti katika michezo ya ligi kuu ambapo baada ya tathmini ya kina wameonekana kuwa wanastahili kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo.

Taarifa iliyochapishwa kutoka katika mitandao ya kijamii ya klabu hiyi ilisomeka kuwa “Wachezaji wetu wawili, @sospeter_bajana04 na @malickou_ndoye, wanatarajia kuondoka nchini Februari 20, mwaka huu, kuelekea jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa majeraha yao”.

Bajana ambaye ni nahodha wa zamani wa klabu hiyo ni tegemeo hasa klabuni hapo katika eneo la kiungo huku Ndoye ambaye husumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara yeye amekua na wakati mzuri pindi anapopata nafasi eneo la ulinzi.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu nchini Azam Fc wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 32 baada ya kucheza michezo 14.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka