Connect with us

Soka

Azamtv wabaniwa kuonyesha Rivers vs Yanga

Kampuni ya Azam media kupitia Azamtv wamenyimwa haki ya matangazo ya mchezo wa marudiano kati ya wenyeji Rivers United ya Nigeria dhidi ya Yanga SC ya Tanzania hatua mtoano.

Azamtv wamesafiri hadi katika mji wa Port Harcourt Nigeria wakiwa tayari kurusha matangazo ya mechi hiyo kwa njia ya televisheni lakini juhudi zao hazijafanikiwa baada ya Rivers United kugoma licha ya Azam media kutoa ofa nzuri.

Katika taarifa yao mkupitia ukurasa wa Instagram wamesema kuwa licha ya uongozi wa Azam media limited kufanya kila namna kununua haki za matangazo hayo kutoka kwa Rivers lakini imeshindikana kwasababu Rivers hawatoonesha mchezo huo mubashara.

Lakini pia Azam media waliomba kurusha matangazo hayo kwa njia ya Radio kupitia Ufm na TV lakini bado Rivers United wamegoma.

Azam kwa hatua hiyo hawataweza tena kurusha matangazo ya mchezo huo lakini watakua wakitoa updates za mchezo kupitia wawakilishi wao walio huko Port Harcourt wakati matangazo ya tamasha la Simba day likiendelea.

Nigeria ni moja kati ya nchi za Africa inayotajwa kuwa na fitina sana za nje ya uwanja linapokuja suala la mechi za kimataifa kwa vilabu na hata timu ya taifa,kwani hata mchezo wa Plateau dhidi ya Simba mwaka jana waligoma kurusha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka