Mshambuliaji Prince Dube amefika katika makao makuu ya Shirikisho la soka nchini (TFF) kwa ajili ya kusikiliza shauri lake dhidi ya Klabu ya Azam Fc ambapo pande hizo mbili zimefika mbele ya kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho hilo.
Dube alifungua madai katika kamati hiyo akidai kuwa haujui mkataba mpya wa miaka miwili anaodaiwa kusaini na Azam Fc kwani mkataba wake unamaliziki Julai 2024 tofauti na wanavyosema Azam Fc kuwa mkataba wake unamalizika 2026.
Dube alifika katika kikao hicho akiwa na mwanasheria wake Respicuis Didas ambaye amefafanua kuwa kiini cha kesi ya mchezaji huyu na klabu yake ya Azam Fc akisema kuwa kesi hii ni ya kimkataba baina ya pande hizo.
“Kwenye system ya Usajili wa Tff inaonyesha Mkataba wa Dube na Azam fc Unamalizika Mwisho wa Msimu huu Ambapo itakuwa julai na Mteja wangu anakuwa huru kujiunga na timu anayotaka.Tatizo Azam Fc.wanasema mteja wangu anamkataba nao hadi 2026 Kila upande umewasilisha vielelezo vyao ngoja tusubiri maamuzi”Alisema mwanasheria huyo.
Azam Fc kwa upande wao wanasema kuwa Mkataba mpya ni ngumu kusajiliwa kutokana na tayari katika mfumo kuna mkataba mwingine huku wakisisitiza kuwa mkataba ni baina ya pande mbili hata kama haujasajiliwa mahali popote.
“Mkataba wa mchezaji kama unaisha 2025, halafu akaongeza mwingine hadi 2028, huo mpya hauwezi kuingia kwenye system hadi ule wa 2025 uishe na huo ndiyo utaratibu”Alisema mkuu wa idara ya Habari ya klabu hiyo Zakaria Thabiti.
Dube amedaiwa kugoma kucheza katika klabu huyo akianza kwa kusingia kuwa ana majeraha na baadae kuandika barua ya kuvunja mkataba wake na klabu hiyo ambapo alirudisha nyumba na gari na kuamua kuondoka klabuni hapo.