Connect with us

Soka

Azam FC,Biashara Utd wajua wapinzani wao CAF

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho la vilabu barani Afrika timu za Azam na Biashara Mara ambazo zimefanikiwa kufuzu hatua ya pili ya mtoano zitakabiliana na wapinzani kutoka Misri na Libya.

Chama cha soka Afrika wametoa ratiba ya michezo ya raundi hiyo ambapo Azam amepangiwa kucheza na Pyramids ya Misri huku wanajeshi wa mapakani Biashara United itakabiliana na Al Ahly Tripol ya Libya.

Timu zote mbili zitaanza michezo ya kwanza nyumbani inayotarajiwa kupigwa kati ya tarehe 15-17 mwezi Oktoba huku michezo ya marudiano ikipangwa kuchezwa kuanzia Oktoba 22-24 mwaka huu.

Azam FC walifanikiwa kusonga mbele baada ya kuwafunga klabu ya Horseed ya Somalia kwa jumla ya mabao 4-1 kwenye michezo miwili huku Biashara wakivuka kwa ushindi wa jumla wa magoli 3-0.

Wawakilishi wengine wa Tanzania Simba SC katika michuano ya klabu bingwa wao watamenyana na Jwaneng FC kutoka Botswana katika hatua ya pili kufuzu makundi ya michuano hiyo.

Kufanya vizuri kwa vilabu hivyo kutaiongezea alama Tanzania na kuiwezesha kuendelea kupeleka wawakilishi wanne katika mashindani ya CAF.

Ratiba kamili ni kama ifuatavyo;

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka