Connect with us

Makala

Azam Fc Yawasili Rwanda

Msafara wa kikosi cha timu ya Azam fc umewasili salama nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa pili wa  hatua za awali za michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya APR Fc ya nchini humo.

Kikosi cha Azam Fc kimewasili nchini humo siku ya alhamis na mapema leo ijumaa kimeanza mazoezi kuikabili klabu hiyo inayomilikiwa na jeshi la nchi hiyo.

Azam Fc itakua na kibarua kikubwa cha kulinda ushindi wa 1-0 ilioupata dhidi ya timu katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza Azam Fc ilipata bao hilo kwa penati iliyopigwa na Jhonier Blanco baada ya Feisal Salum kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.

Azam Fc inapaswa kupata sare ya aina yeyote ile ama isifungwe bao lolote ili kujiweka katika uhakika wa kufuzu hatua inayofuatia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala