Connect with us

Soka

Azam Fc Yawasili Kigoma

Klabu ya Azam Fc imewasili mkoani Kigoma kuwavaa Mashujaa Fc kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc Utakaofanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo.

Azam Fc imewasili ikiwa kamili na mastaa wake wote wa kikosi cha kwanza tayari kwa kutafuta alama tatu baada ya kufungwa katika michezo miwili dhidi ya Yanga sc kwa kipigo cha mabao 3-2 na 3-1 dhidi ya Namungo Fc.

Mashujaa nao pamoja na kuwakaribisha Azam Fc wakiwa nyumbani mkoani Kigoma watakua na kazi kubwa ya kuwafanya ikizingatiwa kuwa wamepoteza michezo miwili mpaka sasa dhidi ya Jkt Tanzania na kipigo dhidi ya Coastal Union katika mchezo wao wa mwisho ugenini mkoani Tanga.

Kocha wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah ‘Bares’ akiwazungumzia wapinzani wao kwenye NBC Premier League hapo kesho amesema kuwa “Mechi itakua ngumu kwa timu zote mbili ukizingatia matokeo ya timu zote katika michezo iliyopita Azam wakifungwa nyumbani na sisi tumepoteza ugenini lakini haijalishi kwa kuwa Azam Fc ina wachezaji bora”.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc Azam Fc ipo katika nafasi ya tatu ya msimamo ikiwa na alama 13 katika michezo saba huku Mashujaa Fc ikiwa katika nafasi tisa ikiwa na alama 8 katika michezo sita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka