Connect with us

Makala

Azam Fc Yamalizana na Taoussi

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kumsainisha mkataba kocha Raia wa Morocco Rachid Taoussi kurithi nafasi ya kocha Yousouph Dabo aliyetimuliwa klabuni hapo.

Taoussi kocha wa zamani wa klabu za Raja Casablanca,As Far Rabat zote za nchini Morocco ambapo mpaka anajiunga na Azam Fc alikua akifundisha timu za vijana za miaka 17,20 na 23 huku pia akiwa mkurugenzi wa Ufundi nchini humo kwa tumu ya wakubwa.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Uongozi wa Azam Fc inasema kuwa kocha huyo ametua sambamba na wasaidizi wake watatu na watakaa klabuni hapo kwa mwaka mmoja.

“Tunayo furaha kumtangaza, Rachid Taoussi, kuwa Kocha Mkuu wetu mpya kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Taoussi, amekuja na wasaidizi wake watatu, Kocha msaidizi, Badr Driss, Kocha wa utimamu wa mwili, Ouajou Driss na Kocha wa makipa, Rachid El Mekkaoui”.Ilisomeka sehemu ya Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia mitandao ya kijamii.

Kabla ya kumnasa kocha huyo Azam Fc ilianza mazungumzo na kocha wa Al Hilal Fc ya nchini Sudan Florent Ibenge ambaye ilishindwana nae katika maslahi huku pia ikijaribu kuzungumza na kocha Juma Mgunda lakini mazungumzo hayo hayakufika mbali.

Azam Fc ilimtimua kocha Yousouph Dabo kutokana na matokeo yasiyoridhisha ambapo alianza kufungwa mabao 4-1 na Yanga sc katika michuano ya kombe la ngao ya jamii kisha akatolewa na Apr ya nchini Rwanda baada ya kukubali kipigo cha 2-0 ugenini katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika na kisha Suluhu dhidi ya Jkt Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ikahitimisha rasmi safari yake ya mwaka mmoja Chamazi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala