Connect with us

Soka

Azam Fc Waipiga Mbeya Kwanza

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Mbeya kwanza katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mchrzo huo uliokuwa wa ushindani kwa pande zote ambazo zilikua zikishambuliana kwa kupokezana na hatimaye dakika za nyongeza kuelekea mapumziko ya kipindi cha kwanza Azam fc walipata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji raia wa Zambia Rodgers Kola aliyeunganisha krosi safi ya Charles Edward Manyama ambaye alipasiwa na kiungo fundi Tepsi Evance na kupiga krosi iliyomkuta mfungaji na kuandika bao la kuongoza kwa Azam Fc.

Licha ya juhudi za Mbeya kwanza kutaka kusawazisha bao hilo lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Azam fc ulihakikisha mchezo unamalizika kwa matokeo hayo na kupelekea kuibuka na alama tatu muhimu ambazo zimewapandisha Azam fc mpaka nafasi ya tano ya msimamo wakiwa na alama 18 katika michezo 12 ya ligi kuu huku mchezo ujao wakikutana na Tanzania Prisons katika uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga.

Mbeya kwanza yenyewe baada ya kupoteza mchezo huo sasa wapo katika nafasi ya 11 wakiwa na alama 11 katika michezo 12 ya ligi kuu huku wakiwakaribisha Kmc siku ya ijumaa januari 21 katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka