Connect with us

Soka

Azam Fc “Out” Mapinduzi Cup

Klabu ya Azam Fc imetolewa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Singida Fountain Gate katika mchezo wa michuano hiyo uliofanyika katika uwanja wa Amani visiwani humo.

Azam Fc ilianza na kikosi kikali kikiwa na mastaa wake wakiongozwa na Yannick Bangala,Paschal Msindo,Daniel Amoah,James Akaminko,Kipre Junior na Yahaya Zayd huku eneo la ushambuliaji likiongozwa na Alasane Diarra.

Azam Fc iltangulia kupachika bao dakika ya  45+3” likifungwa na Allasane Diarra kwa kichwa akipokea pasi ya Pascal Msindo bao ambalo lilidumu mpaka wakati wa mapumziko.

Kipindi cha pili Singida FG walikuja juu na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Elivis Rupia ambaye alipokea pasi nzuri ya Habib Kyombo dakika ya 62 ambapo dakika nne baadae Kyombo alipokea pasi nzuri kutoka kwa Rupia na kufunga kwa kichwa baada ya kufanya shambulizi la kushtukiza langoni mwa Azam Fc.

“Leo tumeshinda kwa sababu tulikuwa wamoja. Mechi ijayo ni ngumu lakini tukiwa wamoja tuna nafasi ya kushinda” alisema Kocha Thabo wa Singida FG.

Singida Fg baada ya kupata mabao hayo mawili walifanikiwa kuyalinda mpaka dakika 90 za mchezo huo zilipokwisha na kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ambapo watakutana na Simba Sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka