Connect with us

Soka

Aucho Afungiwa Mechi 3

Kiungo wa Yanga Sc Khalid Aucho amefungiwa mechi tatu na faini ya laki tano kwa kosa la kumpiga kiwiko nyota wa Coastal Union Ibrahim Ajibi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliozikutanisha Klabu hizo hivi karibuni.

Katika mchezo huo ambao Yanga sc iliibuka na ushindi wa 1-0 staa huyo alikutwa na kosa hilo ambapo mwamuzi Emmanuel Mwandembwa alimpa kadi ya njano.

Taarifa ya kufungiwa kwa staa imetolewa hii leo na kamati ya kusimamia ligi kuu nchini kupitia bodi ya ligi ambapo pia mchezaji huyo amepigwa na faini ya kiasi cha shilingi laki tano za kitanzania.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo ni kuwa adhabu hiyo imetokana na kanuni ya 41:5(5.3) ya udhibiti wa wachezaji ya bodi ya ligi kuu nchini.

Mbali na Aucho pia klabu ya Coastal Union imepigwa faini ya kiasi cha shilingi milioni moja kwa kosa la kuchelewa kutoka katika vyumba vya kubadilishia nguo na kusababisha mchezo huo uchelewe kuanza ambapo adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 17:60 ya ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Pia pilato wa mchezo huo Emmanuel Mwandembwa naye amefungiwa miezi sita kutokana na kushindwa kutafsiri vyema sheria za mpira wa miguu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka