Connect with us

Soka

ATCL:Hatujapokea maombi ya Simba SC

Shirika la ndege nchini ATCL limesema kuwa halijapokea maombi ya safari ya klabu ya Simba kwenda Botswana kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu makundi ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy Oktoba 17 mwaka huu.

Hapo jana bodi ya ligi lilotoa taarifa ya kusogeza mbele mchezo wa ligi kuu kati ya Simba na Polisi Tanzania uliokuwa ufanyike Oktoba 20 hadi Oktoba 27 kutokana na madai ya Simba kuwa wamepata changamoto ya kupata usafiri wa kurudi nchini kutoka Botswana hivyo kuomba mchezo wao wa ligi usogezwe mbele.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Injinia Ladslaus Matindi kupitia mahojiano na radio free Afrika amesema kuwa wao hawajapata maombi ya safari hiyo licha ya wao kuwa wadhamini wa klabu hiyo katika safari za anga,hivyo wanashangazwa na hali hiyo.

Wadau wengi wa soka nchini wamesikitishwa na mabadiliko hayo ya ratiba na kusema ni mapema mno na si ya lazima kwani usafiri kutoka Botswana kurudi nchini ni saa nane tu,hivyo kuusogeza kwa wiki nzima ni makosa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka