Connect with us

Soka

Ansu Fati aibeba Barca dhidi ya Valencia

Kinda wa Barcelona Ansu Fati ameiongoza klabu yake kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Valencia katika mchezo wa ligi kuu soka nchini Hispania(La liga) uliofanyika katika dimba la Camp Nou Jijini Barcelona.

Valencia walikuwa wa kwanza kujipatia bao dakika ya 5 kupitia kwa nahodha wake Jose Gaya,dakika ya 13 Fati aliisawazshia timu yake kwa shuti kali nje ya kumi na nane akimalizia pasi ya mguso kutoka kwa Memphis Depay.

Memphis Depay aliiongezea Barcelona goli la pili kwa mkwanju wa penati dakika ya 41 baada ya Asu Fati kufanyiwa madhambi ndani ya penati box na mlinzi Gaya.

Philipe Coutinho aliyeingia kipindi cha pili aliihakikishia ushindi timu yake kwa kufunga goli la tatu dakika ya 85 na kumaliza ukame wa takribani miezi 11 bila kufunga goli la ligi.

Katika mchezo huo mcshambuliaji mpya wa timu hiyo Sergio Aguero alipata nafasi ya kuichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu ajiunge nayo kutoka Man City akiwa huru.

Barcelona wamepanda ya saba kwenye La liga wakiwa na pointi 15 pointi tano nyuma ya vinara Real Sociedad wenye alama 20 huku Barca wakiwa na faida ya mchezo mmoja mkononi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka