Connect with us

Soka

Aliyekua Kocha Simba Sc Afariki

Aliyekua kocha wa viungo wa klabu ya Simba sc Dr. Adel Zrane amefariki dunia siku ya Jumanne usiku huku sababu ya kifo chake ikiwa utata mpaka sasa ambapo bado mamlaka za serikali zinafanya uchunguzi wa suala hilo.

Kocha huyo aliyekua kipenzi cha mashabiki na wachezaji wa klabu hiyo iliyokua chini ya kocha Patrick Aussems maarufu kama uchebe ambapo mpaka kifo kinamkuta tayari alikua akiifundisha klabu ya APR Fc ya nchini Rwanda ambapo alikutwa amefariki akiwa chumbani kwake.

Kwa mujibu wa mashuhudu nchini humo wanasema kuwa kocha huyo alishiriki katika mchezo wa ligi kuu nchini humo ambao Apr ilitoka sare ya 1-1 na Muhazi United ambapo siku ya jumatatu ilikua ni siku ya mapumziko na siku ya Jumanne wakati dereva anamfata nyumbani kwake kwa ajili ya kwenda mazoezini ndipo alimkuta amefariki.

Mpaka sasa tayari Mamlaka ya uchunguzi nchini Rwanda(RIB) inaendelea na uchunguzi kuhusu kifo cha kocha huyo huku taratibu za kuusafirisha mwili huo kwenda nchini kwa Tunisia zikiwa zinaendelea.

Zrane mwenye miaka 40 kabla ya kujiunga na klabu hiyo alitoa huduma katika klabu na timu za taifa mbalimbali kama vile Simba sc,timu ya Taifa ya Mauritania huku timu yake ya Apr ikisitisha michezo yake kwa muda mfupi kwa ajili ya maombolezo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka