Baada ya kuwasili nchini Kikosi cha Al Ahly Sc kimefanya mazoezi ya mwisho hii leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa tayari kwa kuwakabili Young Africans hapo kesho Jumamosi.
Kikosi hicho ambacho kiliwasili alfajiri ya leo kikiwa na kila kitu chake kutoka nchini humo ikiwemo chakula na maji ya kunywa mapema baada ya mkutano na vyombo vya habari kiliamua kufanya mazoezi mchana wa jua kali ili kuifanya miili kuzoea joto.
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo muhimu kwa Yanga kwa ajili ya kufufua matumaini yao katika mashindano hayo makubwa Afrika, Gamondi amesema hawataruhusu makosa waliyofanya dhidi ya CR Beloizdad.
“Tunafahamu tunacheza na klabu kubwa Afrika, hatutaruhusu makosa kama yale tuliyofanya kwenye mchezo wetu uliopita, hizi timu kubwa ukifanya makosa kidogo tu unaadhibiwa tofauti na kwenye ligi ya ndani, unaweza kufanya makosa na usiadhibiwe,” alisema Gamondi.
“Shida yetu ni kupata pointi tatu hapa nyumbani, hiyo ni lazima” Alisema Nahodha wa Yanga SC, Bakari Nondo Mwamnyeto akieleza malengo yao kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly.
Yanga sc inapaswa kushinda mchezo huo hasa baada ya timu ya medeama kufanikiwa kuifunga 2-1 timu ya Cr Belouzdad na kulifanya kundi hilo D kuwa gumu zaidi kwa Yanga sc ambao mpaka sasa ni wanashika mkia katika msimamo.