Connect with us

Soka

Aiyee Atua Kmc

Mshambuliaji wa Mwadui Fc Salim Aiyee ametua katika klabu ya Kmc kwa mkataba wa miaka miwili akitokea timu hiyo ya mjini shinyanga.

Mshambualiaji huyo aliyeisaidia Mwadui kubaki ligi kuu Tanzania katika michezo miwili ya mtoano dhidi Geita gold mine  amesaini kandarasi hiyo ya kujiunga na timu hiyo inayomilikiwa na Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni.

Aiyee katika msimu wa ligi kuu msimu ulioisha alifunga jumla ya magoli 18 yaliyomfanya kuwa katika orodha ya wafungaji bora akizidiwa na Meddie Kagere aliyefunga mabao 23.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka