Connect with us

Soka

Adebayor Kupishana na Saido Simba sc

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba sc ni kwamba klabu hiyo ina mpango wa kuachana na staa wake Saido Ntibanzokiza ambapo nafasi hiyo itazibwa na mshambuliaji Victorien Adebayor ambaye atatua klabuni hapo katika dirisha dogo la usajili mwezi ujao.

Mkataba wa Saido na Simba sc uko ukingoni ambapo mpaka sasa mazungumzo ya mkataba mpya yakiwa bado hayajaendelea huku staa huyo akiwa ni mmoja ya wachezaji waliopelekwa katika kamati ya maadili ya klabu hiyo akihisiwa kuwa amehujumu timu katika mchezo dhidi ya Yanga sc ambapo walifungwa 5-1.

Mbali na kuachana na staa huyo Simba Sc pia Saido Ntibazonkiza ambaye mkataba wake unaisha mwezi ujao pia klabu hiyo  imepanga kusajili wachezaji 2 wakigeni kwenye dirisha dogo la usajili ambao ni Adebayor pamoja na Cesar Manzoki ambaye walishindwa kumsajili msimu uliopita.

Simba sc inapaswa kuboresha zaidi kikosi chake kwa inakabiliwa na ratiba ngumu ya michuano ya kimataifa ambapo itaanza kampeni dhidi ya Asec Mimosas siku ya novemba 25 mwaka huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka