Connect with us

Soka

Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba kwa kuwashinda wenzie Mohamed Salah,Joao Cancelo,Sarr,Rudiger na Saint Maxim.

Ronaldo aliifungia Man Utd magoli matatu katika michezo mitatu ya ligi hiyo ndani ya mwezi huo na kuisaidia timu yake kufikisha alama 14 kwenye ligi hiyo.

Hii ni tuzo ya tano kwa Ronaldo ya mchezaji bora wa mwezi wa  ligi hiyo,huku tuzo yake ya mwisho akiichukua miaka 13 iliyopita kabla ya kutimkia Hispania kukipiga Real Madrid.

Wakati huo huo kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta amechukua tuzo ya mwezi huo baada ya kuwashinda Pep Guardiola,Jurgen Klopp,Graham Potter na Dean Smith

Arteta Asenal kushinda michezo mitatu mfululizo ya mwezi huo huku wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara moja tu katika michezo hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka