Connect with us

Soka

Messi aibeba PSG,Madrid wakishangazwa UCL

Mshambuliaji wa PSG usiku wa kuamkia leo ameibeba timu yake hiyo katika ushindi  wa magoli 2-0 dhidi ya Manchester city katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya.

Katika mchezo huo uliofanyika katika dimba la Parc de Prince jijini Paris,PSG ilijipatia goli lake la kwanza dakika ya 30 kupitia kwa Gana Gueye  aliyepiga shuti la juu juu lililomshinda mlinda mlango wa Man City Ederson na kuipa uongozi timu yake katika kipindi cha kwanza.

Man city walikuwa na siku mbaya ofisini baada ya kushindwa kuweka mpira kambani licha ya kuengeneza nafasi za kutosha,dakika ya 80 mchawi wa soka Messi alilizamisha jahazi la city kwa shuti kali akimalizia pasi ya kugusa kutoka kwa Mbappe na kufungua akaunti yake ya mabao katika timu yake hiyo mpya.

Katika mchezo mwingine mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo Real wameduwazwa na washiriki wapya wa michuano hiyo klabu ya Sheriff kutoka Moldova kwa kichapo cha 2-1 nyumbani Santiago Bernabeu katika mchezo uliowashangaza wengi.

Matokeo mengine ya UCL hapo jana ni kama ifuatavyo;

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka