Connect with us

Makala

16 Kushiriki Kagame Cup

Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza kwamba klabu 16 zitashiriki michuano ya Kagame Cup inayotarajiwa kuanza Julai 6 hadi 22 mwaka huu Visiwani Zanzibar.

Katika Taarifa iliyotolewa kwenda kwa umma na Cecafa imeonyesha kwamba katika michuano ya mwaka huu jumla ya timu 16 zitashiriki huku timu za  TP Mazembe (DR Congo), Nyasa Big Bullets (Malawi) na Red Arrows FC ya Zambia zote zimethibitisha ushiriki wao kujiunga na timu 13 nyingine kutoka Ukanda wa CECAFA.

Awali michuano hiyo ilipangwa kufanyika nchini Sudan lakini kutokana na hali ya kisiasa kutotengemaa basi iliwalazimu Cecafa kuihamishia michuano hiyo Zanzabar huku Sudan wakipewa nafasi ya kuingiza timu nne kama mwenyeji ambapo timu za El Merreikh, Al Hilal, Hai El Wadi zitashiriki huku Tanzania ikiingiza timu za Simba sc,Yanga sc,Azam Fc na Coastal union na Rwanda ikiingiza timu ya APR na Vital O kutoka nchi ya Burundi itashiriki.

Timu nyingine ni Gor Mahia (Kenya), SC Villa (Uganda), JKU SC (Zanzibar), El Merreikh FC-Bentiu (Sudan Kusini), Nyasa Big Bullets (Malawi), TP Mazembe (DR Congo) na Red Arrows (Zambia) ambazo zitaungana na timu alikwa kuunda timu 16 zitakazoshiriki michuano hiyo inayodahminiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

“Mashindano haya yatasaidia timu zetu katika ukanda huu kujiandaa vizuri kabla ya msimu wa CAF Champions League na CAF Confederation Cup 2024/2025 ambao unaanza mwezi Agosti. Kuwa na timu kubwa kutoka DR Congo, Malawi na Zambia pia kutapa msisimko kwenye mashindano yetu na kutoa changamoto halisi kwa timu zetu,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA, John Auko Gecheo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala