Connect with us

Soka

Mayay Afunguka Ujenzi Uwanja Arusha

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Ally Mayay amesema waandaaji wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027; Tanzania, Kenya na Uganda kila nchi itapaswa kuwa na viwanja vitatu na hivyo maandalizi ya kujenga uwanja wa tatu jijini Arusha tayari yameshaanza.

Mayay alisema kuwa viwanja vitakavyotumika katika michuano hiyo ni uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam,Uwanja wa Amani visiwani Zanzibar na uwanja mpya ambao ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi machi mwaka huu jijini humo.

Mayay amesema mambo ya tathimini yalishakamilika na sasa wako katika hatua ya mapatano, na kwamba ujenzi wa uwanja huo mpya wenye uwezo wa kubeba watu 30,000 utaanza kujengwa mwezi ujao.

“Tuko kwenye hatua za mwisho na mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa Arusha, mpaka Desemba 2025 CAF watakuja kuangalia tayari utakuwa umekamilika.”

Amesema hayo leo Februari 14, 2024 wakati akichangia mjadala wa Mwananchi Space ulioandaliwa na Mwananchi Communications Ltd, wenye mada isemayo “Tanzania imejifunza nini kupitia AFCON 2023, ikijiandaa 2027?”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka