Connect with us

Soka

Mabosi wa Al Hilal Fc ya Sudan wamevutiwa na uwezo wa kiungo mshambuliaji na nahodha wa KMC Awesu Awesu hivyo muda wowote yawezekana mazungumzo ya kumsajili yakaanza ili ajiunge nao katika usajili wa dirisha dogo mwezi ujao.

Mabosi hao walikuwepo katika mchezo wa kirafiki baina ya timu hizo uliofanyika katika uwanja wa Baobab na kufanikiwa kuvutiwa na uwezo wa kiungo huyo mshambuliaji wa zamani wa Kagera Sugar na Azam Fc.

Kocha Frolent Ibenge anaona kama Awesu atakua chaguo sahihi katika kuongeza ubora wa safu yake ya kiungo msimu huu hasa katika michuano ya kimataifa.

Mabosi wa Kmc Fc wanasubiri ofa kutoka kwa Al Hilal kuona kama wanaweza kumuachia staa huyo kujiunga na timu hiyo mpya kutokana na ukweli kwamba atapata maslahi mazuri kama mchezaji huku timu pia itapata faida.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka