Connect with us

Soka

Stars Yawasili Morocco

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imewasili nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger utakaochezwa kwenye mji wa Marrakech Jumamosi Novemba 18, 2023.

Stars imewasili nchini humo ikiwa na mastaa wake kamili tayari kwa mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi ambapo Stars ipo kundi E na timu za Congo Dr,Zambia,Morocco na Niger ambapo Stars inapaswa kushinda mchezo huo kabla ya kuwavaa Morocco siku ya Jumanne jijini Dar es salaam.

Asilimia kubwa ya mastaa waliosafiri na kikosi hicho ni wale waliokuwepo wakati wa mchezo wa kufuzu Afcon dhidi ya Algeria ambapo walioongezeka katika orodha hiyo ni kipa Aishi Manula,Matheo Anthony pamoja na mastaa wa kitanzania wanaocheza ulaya kama Ibrahimu Joshua, Omar Mvungi,Baraka Majogoro,Charles M’muobwa kutoka klabu ya Macarthur FC ya Australia na Kwesi Kawawa.

Kocha Adel Amrouche ameamua kutumia wachezaji wa kitanzania waliopo nje ya nchini wakisakata soka ili kuongeza uzoefu na ushindani katika kikosi cha Stars ambacho mwakani kitashiriki michuano ya mataifa ya Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka