Connect with us

Soka

10BET yafanya ukarabati Jamhuri Dododma

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya 10BET inayoidhamini klabu ya soka ya Dodoma Jiji imeamua kufanya ukarabati katika dimba la Jamhuri Dodoma uwanja wa nyumbani wa timu hiyo.

Ukarabati huo umehusisha matengenezo ya vyumba vya kubadilishia nguo kuwa vya kisasa zaidi,vyoo vya uwanjani hapo pamoja na muonekana mzima wa uwanja huo japo haijawekwa wazi kama utahusisha na eneo la kuchezea.

                                                                                                         

Matengenezo ya vyumba vya kubadilishia nguo kwa wachezaji kunaufanya uwanja huo kuwa moja kati ya viwanja bora vitatu nchini kwenye eneo hilo ukitanguliwa na Benjamin Mkapa na Chamazi.

Uwanja huo tayari umeshaanza kutumia kwa mechi za usiku baada ya kuwekea taa hivyo ukarabati huo utauongezea hadhi na endapo eneo la kuchezeo litawekwa sawa basi utakuwa moja kati ya viwanja bora nchi ukuzingatia upo mako makuu ya nchi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka