Connect with us

Masumbwi

Wilder vs Fury kuzichapa oktoba 9

Pambano la masumbwi kati ya Mmarekani Deontay Wilder dhidi ya Muingereza Tyson Fury limepangiwa upya tarehe,sasa kupigwa oktoba 9,2021.

Pambano hilo la tatu la mabondia hao awali lilipangwa kufanyika Julai 24 Las Vegas, lakini lililazimika kuahirishwa mara baada ya Fury kupata maambukizi ya covid-19. Fury 32,alimpiga Wilder 35 Februari mwaka 2020 na kushinda ubingwa wa uzito wa juu wa WBC.

Wote wawili hawajapanda tena ulingoni tangu walipopigana wenyewe mwaka 2020.

Fury alisema ”siihitaji chochote zaidi ya kumpiga huyo mvivu Julai 24 lakini kichapo kitabidi kisubiri, hakuna tatizo nitarudi nikiwa imara zaidi,tutapigana oktoba 9 na nitamwangusha tena”.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Masumbwi