Connect with us

Masumbwi

Kiduku kurudi Ulingoni

Bondia Twaha kiduku anatarajiwa kurudi ulingoni mwezi ujao tarehe 26 kukipiga na bondia Alex Kabungu katika pambano la ubingwa ambalo litafanyika mkoano Morogoro.

Bondia huyo ambaye mara ya mwisho alipanda ulingoni Agosti mwaka jana akifanikiwa kumpiga Dulla Mbabe amekubali kucheza pambano hilo na Bondia huyo wa kimataifa kutoka Congo Drc.

“Ni kweli nimesaini kucheza pambano hilo ambalo litakuwa la mkanda wa ubingwa, naamini mkanda utabakia kwa sababu lazima nifanye maandalizi ya kutosha chini ya kocha wangu Pawa Ilanda.

“Kila kitu tayari kimeshapangwa na promota juu ya siku ya pambano lakini maombi yangu ni kuweza kuwezasha pambano kufanyika mjini ili watu wengi waweze kuhudhuria taofauti na Magadu kwa sababu ni mbali na mjini,”Alisema Kiduka ambaye makazi yake ni mkoani Morogoro.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Masumbwi