Connect with us

Masumbwi

Bondia Mnemwa Aomba Msaada

Kufuatia kupigwa na kujeruhiwa vibaya alipokua ulingoni katika pambano la ngumi la raundi nne dhidi ya Ally Sewe katika ukumbi wa Mrina Manzese Tiptop,bondia Mohammed Mnemwa ameita wadau kumsaidia gharama za matibabu katika Hospitali ya Muhimbili alipolazwa.

Bondia huyo amelazwa baada ya vipimo vya CT Scan kuonyesha kuwa anasumbuliwa na tatizo la damu kuvilia katika ubongo baada ya kupigwa ngumi kali katika pambano hilo.

Baada ya kufikishwa Hospitalini hapo bondia huyo amezungumza kwa mara ya kwanza na kuomba msaada.

“Mimi kwa hali yangu nilikua naomba watu wajitokeze serikali kama hivyo vyama vya ngumi wanisaidie kwa gharama zitakazotajwa hapa ili niendelee kurudi kwenye michezo yangu kwasababu ngumi ndio maisha yangu ambayo nimejichagulia”,Alisema kwa huzuni bondia huyo.

“Kama misaada kama mtu yeyote mwenye uwezo watu wanaonijua waandaaji wa mapambano wasimamizi lazima wasogee kama kuja kuniona na watahusika na chochote kitu ili mwenyewe niweze kuinuka tena niendelee na shughuli zangu sasa hivi nasikia maumivu kwenye kichwa”,Alimalizia kusema Mnemwa.

Mnemwa alipigwa katika raundi ya tatu katika pambano hilo lenye raundi nne na kupoteza pambano hilo.

 

Bondia huyo kwasasa anapatiwa matibabu kwenye taasisi ya mifupa MOI iliyopo chini ya hospital ya Taifa ya Muhimbili ambapo baada ya vipimo alivyofanyiwa awali aligundulika na tatizo la damu imevilia kwenye ubongo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Masumbwi