Connect with us

Masumbwi

Anthony Joshua,Kibonge kurudiana Desemba

Baada ya kuishangaza dunia kwa kumchapa Anthony Joshua,Bondia Andy Ruiz Jr amekubali kurudiwa kwa pambano lake na bondia huyo kati ya mwezi Novemba au Desemba mwishoni mwa mwaka huu.

Joshua atapata nafasi ya kurudisha mikanda yake ya uzito wa juu ya IBF,WBA,WBO aliyoipoteza baada ya kupigwa na bondia huyo raia wa Mexico mwenye miaka 29 aliyepigana mapambano rasmi 34 na kushinda 33 huku 22 akishinda kwa kumuangusha mpinzani wake mapema kabla ya pambano kuisha (knouck out).

Taarifa za kurudiwa kwa pambano hilo zilithibitishwa na promota Eddie Hearn kwamba kipengele cha kurudiana kwa pambano hilo kimeafikiwa na pande zote mbili japo bado kuna utata kuhusu mahali ambapo pambano hili litafanyakia baada ya Joshua kutaka lifanyike Uingereza na Andy akihitaji lifanyike nchini Mexico.

Joshua alikutana na kipigo cha kwanza katika maisha yake ya ndondi baada ya kupigwa na bondia huyo licha ya watu wengi kutompa nafasi hasa baada ya kuwa kibonge na kuonekana dhaifu.Mzaliwa huyo wa uingereza alisema hakudhani kama kulikua na kipengere cha kurudiwa kwa pambano hilo maana aliamini atashinda.

Joshua alipoteza pambano hilo siku ya jumapili alfajiri katika raundi ya saba,pambano lilifanyika katika ukumbi wa madison square nchini marekani na kuwa pambano la kwanza kupoteza kwa Joshua katika historia yake baada ya kucheza mapambano rasmi 23 na kushinda 22 huku 21 akishinda kwa knock out.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Masumbwi

  • Mwakinyo Huru

    Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBRC) imemfungulia bondia Hassan Mwakinyo kutoka kifungoni baada...

  • Bondia Mtanzania Fadhili Majiha ‘Kiepe Nyani’ ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBC Afrika...

  • Ibrahim Class Amtwanga Mchina

    Bondia Mtanzania Ibrahim Class ameshinda pambano la ubingwa wa TPBRC dhidi ya bondia raia...

  • Mwakinyo Aitwa Mahakamani

    Kampuni ya PAF Promotion imemfungulia shauri la madai Bondia Hassan Mwakinyo ambalo linatarajiwa kutajwa...