Connect with us

Makala

Yanga Yatetema Afcon Misri

Yanga sc imeendelea kuonyesha umwamba katika kufanya usajili baada ya kumalizana na nyota kadhaa ambao wapo katika michuano ya Afcon nchini Misri ili kuwahi kutuma majina shirikisho la soka barani Afrika(Caf) ambalo limetangaza mwisho kutuma majina ni 30 june mwaka huu.

Msafara wa viongozi wa kamati ya usajili wa klabu hiyo ukiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya hiyo Frank Kamugisha imekamilisha usajili wa Ally Mtoni Sonso na kipa kutoka Kenya Farouk Shikalo ambao ni pendekezo la mwalimu Zahera.

Farouk Shikalo akisaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo.

Kukamilika kwa usajili wa wachezaji hao ambao walianza mazungumzo na yanga kabla ya kwenda kwenye michuano hiyo mikubwa afrika kumefanya usajili wa timu hiyo kukamilika kwa zaidi ya asilimia 95 na kubaki sehemu ndogo tu kwa mujibu wa mwenyekiti wa timu hiyo Dk.Mshindo Msolla.

Mabingwa hao mara 27 wa taji la ligi kuu Tanzania bara watawatambulisha rasmi wachezaji hao siku ya tamasha la wiki ya Mwananchi ambalo litazinduliwa rasmi mwaka huu na litakuwa endelevu kila mwaka na kutakua na mchezo maalumu wa kimataifa wa kirafiki.

Pia klabu hiyo imetoa onyo kwa watu wanauza bidhaa zenye nembo ya klabu hiyo pasipo kufata taratibu rasmi kuwa mwisho ni june 30 mwaka huu na imewataka kufika klabuni hapo kupewa utaratibu maalumu utakaokuwa na manufaa kwa klabu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala