Connect with us

Makala

Yanga Yaibuka Na Ushindi Singida United

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael  amesepa na pointi tatu muhimu kwa mara ya kwanza kwa ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Singida United katika uwanja wa Namfua.

Molinga alipachika bao la kwanza dakika ya 12 na kipindi cha pili waliongeza juhudi na kufunga bao la pili kupitia kwa Haruna Niyonzima dakika ya 57 akimalizia pasi ya Morison.

Wakati mabeki wa Singida United wakijitahidi kuokoa mpira ulio ndani ya 18 mchezaji wa Yanga Yikpe aliongeza bao la tatu dakika ya 77 huku Singida United wakijipatia bao la kufuta machozi dakika ya 82 kupitia Six Mwakasege. .

Luc Eymael alisema kuwa walijipanga kupata ushindi na hivyo ahadi imetimia kwa mashabiki wa Yanga.’8

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala