Connect with us

Makala

Yanga Yaahidi Kurekebisha Makosa Jumatano

Nahodha msaidizi wa Yanga Juma Abdul ameahidi kuwa watapambana vya kutosha katika mechi zilizobaki na kurekebisha makosa yaliyowafanya wakapoteza michezo miwili ya nyuma.

Yanga ambayo ilipoteza mchezo mbele ya Kagera Sugar kwa kichapo cha mabao 3-0 na mbele ya Azam Fc kwa kichapo cha bao 1-0 wamewaomba wananchi na mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa tarehe 22 Januari 2020 dhidi ya Singida United katika uwanja wa Namfua.

Kikosi cha Yanga kwa sasa kipo nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 14 huku singida united ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 10.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala