Connect with us

Makala

Yanga sc Yatozwa Faini 5m

Klabu ya Yanga sc imetozwa faini ya kiasi cha shilingi milioni tano za kitanzania kutokana na kosa la kutumia mlango usio rasmi wakati wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba sc siku ya Jumapili Oktoba 23 jijini Dar es salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Kwa mujibu wa taarifa kwa Vyombo vya habari iliyotolewa na bodi ya ligi kuu nchini imesema kuwa kikao cha tathmini kuhusu mwenendo wa ligi kuu nchini kilichofanyika Novemba 4 kilipitia ripoti mbalimbali za michezo na kukuta kosa hilo la Yanga sc na kuamua kuwapa adhabu hiyo kwa uzingativu wa kanuni ya 17:(21&60) kanuni inayohusu taratibu za mchezo.

Hii si mara ya kwanza kwa Yanga sc kupewa adhabu kama hizi za faini ambapo imepewa adhabu hata katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Simba sc kutokana na kutofuata taratibu za mchezo ikiwemo kupitia katika milango isiyo sahihi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala