Connect with us

Makala

Yanga sc Yatinga Robo Fainali

Klabu ya Yanga sc imeingia hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuifunga klabu ya Biashara United 2-1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Yanga sc ilianza mchezo ikiwa na hasira baada ya kutoa suluhu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Mbeya City ilipata nafasi nyingi za mapema lakini ilishindwa kuzitumia huku bao la Fiston Mayele likikataliwa na mwamuzi kwa madai ya kwamba ameotea.

Yanick Bangala aliitanguliza Yanga sc dakika ya 22 ya mchezo huku Fiston Mayele baada ya dakika sita na kufanya mashabiki wa Yanga sc uwanjani kujawa na furaha isiyo kifani japo ilifutika dakika ya 37 baada ya Biashara United kufunga bao la kwanza kutokana na uzembe wa Khalid Aucho kuokoa mpira wa krosi.

Yanga wanaungana na Polisi Tanzania,Kagera Sugar na Coastal Union katika orodha ya timu zilizofuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala