Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Klabu ya Cbe SA ya nchini Ethiopia katika mchezo wa marudiano wa hatua ya pili ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika uliofanyika katika uwanja wa New Amaan complex Visiwani Zanzibar.
Yanga sc ikiingia na ushindi wa 1-0 ilioupata katika mchezo wa kwanza nchini Ethiopia ambapo iliwachanganya Wa Ethiopia hao kwa kuwapumzisha mastaa wake wa kikosi cha kwanza Stephen Aziz Ki,Khalid Aucho na Prince Dube na kuwaanzisha Clement Mzize na Cletous Chama kama washambuliaji wakisaidiwa na Pacome Zouzoua,Maxi Nzengeli,Jonas Mkude na Mudathir Yahaya huku eneo la ulinzi wakianza Djigui Diarra,Yao Kouasi,Chadrack Boka,Dickson Job na Ibrahim Hamad Bacca.
Chama aliitanguliza Yanga sc dakika ya 35 ya mchezo mwishoni mwa kipindi cha kwanza akimpiga chenga kali kipa wa Cbe baada ya kupokea pasi safi ya Mudathir Yahaya na kufunga bao hilo la uongozi huku mapema kipindi cha pili dakika ya 47 Clement Mzize alifunga bao la pili kwa Yanga sc akimalizia kazi nzuri Mudathir Yahaya.
Mabadiliko ya mwalimu Gamondi ya kumuingiza Aziz Ki na Dube yalianza kulipa baada ya Ki kufunga bao la tatu dakika ya 74 ya mchezo akimalizia kwa shuti kali mpira uliookolewa vibaya na mabeki wa Cbe.

Dakika ya 88 Mudathir Yahaya alifunga bao la nne kwa Yanga sc kwa shuti kali huku dakika mbili baadae Duke Abuya nae alifunga bao kali na Azizi ki alihitimisha bao la sita kwa Yanga sc akiwachambua mabeki wa Cbe na kuifanya Yanga sc kufuzu kwa jumla ya mabao 7-0 pamoja na lile la mchezo wa kwanza.
Yanga sc pamoja na kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika pia ilijishindia shilingi milioni 30 za goli la mama ambazo hutolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Samia Suluhu Hassan.