Connect with us

Makala

Yanga sc Yatangaza Viingili Cafcl

Klabu ya soka ya Yanga sc imetangaza viingilio vy amchezo wake wa kwanza wa hatua ya awali katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Asas Fc ya nchini Djibout utakaofanyika siku ya Jumapili August 20 katika uwanja wa Chamazi Complex.

Akizungmza na waandishi wa habari mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo Ally Kamwe alisema kuwa kutokana na mipango ya uongozi kiingilio cha juu kitakua kiasi cha shilingi elfu thelasini na kiingilio cha chini kitakua ni elfu tano tu katika eneo la mzunguko.

“Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha Wanahabari na Mashabiki wetu wote wanaotufatilia Mubashara kupitia Azam TV na leo nimekuja kuwapa taarifa za Mashindano ya Kimataifa na Hali ya Kikosi chetu baada ya mechi ya fainali Ngao Jamii,

Tutacheza mchezo wetu wa kwanza hatua ya awali CAFCL dhidi ya ASAS Djibouti kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi tarehe 20.08.2023 majira ya saa 11:00 jioni” Ally Kamwe
“Viingilio vya mchezo wetu wa kwanza, Jumapili dhidi ya ASAS Djibouti kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ni VIP A – tsh 30,000,VIP B – tsh 20,000 na mzunguko – tsh 5,000 na kuanzia sasa tiketi zimeshaanza kuuzwa Makao Makuu ya Klabu Jangwani na tutatangaza vituo vingine kupitia mitandao yetu ya kijamii”.
Yanga sc imepata bahati ya pekee katika michezo hiyo ya hatua za awali ambapo michezo yote itafanyika katika uwanja wa Chamaza jijini Dar es salaam kutokana na sababu kwa timu hiyo ya Asas Fc kutoka nchini Djibout imekosa uwanja wenye hadhi ya Caf nchini mwao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala