Connect with us

Makala

Yanga Sc Yapaa Afrika

Shirikisho la kimataifa la historia na takwimu za mpira Duniani (IFFHS) limetangaza vilabu bora Africa ndani ya mwaka mmoja kuanzia Septemba 30 2022 mpaka August 31 2023.

Katika orodha hiyo mpya klabu ya Yanga sc imeshika nafasi ya tatu barani Afrika ikiwa na alama 145.5 huku ikianguliwa na klabu za Al Ahly Fc yenye alama 236 na Wydad Casablanca wenye alama 155.5 huku katika upande wa Dunia Yanga sc imeshika nafasi ya 63.

Takwimu hizo za ubora wa klabu zimechukuliwa kuanzia Septemba 30 2022 mpaka August 31 mwaka huu ambapo wanaangalia ubora katika mashindano yote ambayo klabu inakua imeshiriki kwa wakati husika.

Yanga sc katika kipindi hicho ilifanya vizuri katika michuano ya ligi kuu ya Nbc ambapo walikua mabingwa huku pia wakichukua kombe la ngao ya jamii na kombe la shirikisho la Azam huku wakifika fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

IFFHS ni shirika la takwimu za soka duniani na linatambuliwa na shirikisho la soka duniani yaani Fifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala