Connect with us

Makala

Yanga sc Yanusa Makundi CAFCL

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 upo uwezekano wa klabu ya Yanga sc kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al-Merrikh ya nchini Sudan.

Yanga sc imepata ushindi huo katika mchezo uliofanyika jijini Kigali katika uwanja wa Pele Nyamirambo ambapo Wasudan hao walikua wenyeji wa mchezo huo.

Kocha Gamondi alianza na kikosi chenye mabadiliko akiwaanzisha pamoja Pacome Zouzou,Aziz Ki na Max Nzengeli huku Mudathir Yahaya na Khalid Aucho wakisimama eneo la katikati mwa uwanja na Dickson Job,Ibrahim Hamad,Yao Kouasi na Joyce Lomalisa wakiwa kama walinzi wakiongozwa na Djigui Diara.

Clement Mzize aliyekua kama mshambuliaji pekee alikosa nafasi kadhaa za kufunga hasa kipindi cha kwanza ambapo kipindi cha pili uamuzi wa kocha Gamondi kumuingiza Kennedy Musonda ulizaa matunda baada ya kufunga bao la kwanza akiunganisha kwa kichwa krosi ya Pacome Zouzou dakika ya 60 ya mchezo.

Akiwa katika kiwango kizuri kabisa Stephane Aziz Ki alifanikiwa kumpa pasi nzuri Clement Mzize dakika ya 78 na kuandika bao la pili la mchezo huo.

Yanga sc sasa inapaswa kulinda ushindi huo wakati wa mchezo wa marudiano utakaofanyika nchini Septemba 30 mwaka huu katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam ambapo wakifanikiwa itakua wamefuzu makundi ya ligi ya mabingwa baada ya miaka 25 kupita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala