Connect with us

Makala

Yanga sc Yanusa Fainali Cafcc

Klabu ya Yanga sc imenusa mguu mmoja kuingia fainalki ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga 2-0 klabu ya Marumo Gallants ya nchini Afrika kusini katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jumatano ya Mei 10.

Yanga sc ikicheza kwa mkakati maalumu wa kuzuia na kushambulia mara chache chache ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa haijapata bao huku ikiwa na mchezo usiowafurahisha mashabiki wengi huku wachezaji kama Tuisila Kisinda na Stephane Aziz Ki wakishindwa kuumuda mchezo wakipoteza pasi mara kwa mara.

Yannick Bangala alipiga pasi nzuri kwa Tuisila Kisinda aliyeingia kwa nguvu ndani ya eneo la hatari na kumpasia Aziz Ki aliyefunga bao la uongozi dakika ya 64 ya mchezo ambapo baada ya bao hilo Kocha Nasredine Nabe aliamua kufanya mabadiliko akiwatoa Jesus Moloko,Yannick Bangala,Tuisila Kisinda na Aziz Ki akiwaingiza Mudathir Yahya,Salum Abubakar,Clement Mzize na Benard Morrison.

Kuingia kwa wachezaji hao kuliwafanya Yanga sc kumiliki mchezo na kuwanyima nafasi Gallants waliokua na mshambuliaji hatari Ranga Chivahiro mwenye mabao matano katika michuano hiyo na mabao kumi ya ligi kuu ya Afrika kusini ambapo pia viungo kama Lucky Mohomi na Sibosiso Nkosi walikosa umakini baada ya kuzidiwa maarifa na viungo wa Yanga sc.

Fiston Mayele aliunasa mpira uliokuwa umeokolewa kutoka katika kona langoni mwa Yanga sc akiwa amebaki na mlinzi mmoja na kumpasia Benard Morrison ambaye alifunga bao la pili kwa Yanga sc katika dakika ya pili ya nyongeza baada dakika tisini kutamatika.

Yanga sc sasa imetanguliza mguu mmoja katika hatua ya fainali ya michuano hiyo ya kombe la shirikisho ambapo inapaswa kushinda ama kupata sare yeyote au kufunga chini ya mabao mawili ili kufuzu hatua ya fainali ambapo itaweka historia kubwa ya kuwa timu ya kwanza kucheza fainali ya michuano mikubwa ya Caf hapa nchini kwa miaka ya hivi karibuni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala