Connect with us

Makala

Yanga sc Yamtambulisha Mrithi wa Mayele

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Hafiz Konkoni kutoka klabu ya Benchem Fc inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ghana kwa mkataba wa miaka miwili kuja kuchukua nafasi ya Fiston Mayele ambaye amejiunga na Pyramids Fc ya nchini Misri.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 23 alitua nchini siku ya Jumamosi kukamilisha dili hilo na sasa ametambulishwa rasmi kama msjambuliaji kiongozi wa klabu hiyo kuchukua nafasi ya Mayele klabuni hapo.

Hafiz mwenye umbo kubwa huku akiwa na sifa ya unyambulifu ametoka ligi kuu ya Ghana akiwa na rekodi ya kufunga mabao 15 katika michezo 29 ya ligi kuu huku akifunga mabao 34 katika michezo 97 kwa misimu minne aliyokaa klabuni hapo.

Klabu za Hearts of Oak, Asante Kotoko na baadhi ya klabu barani ulaya zilikua zinamuwania mshambuliaji huyo ikizingatiwa ana umri sahihi wa kwenda ulaya lakini Yanga sc imefanikiwa kumsajili na tayari ameshajiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo Avic Town Kigamboni.

Hafiz anatarajiwa kuiongoza Yanga sc katika michuano ya ngao ya jamii inayoanza Augusti 8 ambapo Yanga sc itavaana na Azam Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala