Connect with us

Makala

Yanga sc Yamkalisha Mwarabu kwa Mkapa

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Us Monastry katika mchezo wa kombe la shirikisho uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi za vilabu barani Afrika.

Ikicheza mbele ya takribani mshabiki elfu 30 Yanga sc iliukamata mchezo huo mwanzo mwisho huku ikipeleka mashambulizi kwa kasi kiasi cha kipa Sadok Yeddes kulazimika kufanya jitihada za makusudi kuokoa michomo mikali ya Fiston Mayele na Djuma Shabani.

Kennedy Musonda alianza kuipatia bao Yanga sc dakika ya 33 ya mchezo kwa kichwa kikali akimalizia krosi ya Jesus Moloko baada ya kazi nzuri ya Khalid Aucho ambapo bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza kinaisha.

Kocha Nabi baada ya maelekezo Yanga sc katika vyumba vya kubadilishia nguo kilichofata kwa wachezaji ni utekelezaji wa mipango ambapo Fiston Mayele alifunga bao la pili dakika ya 59 na la mwisho katika mchezo huo mpaka dakika 90 zinaisha na kuihakikishia Yanga sc ushindi na kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Yanga sc sasa imefikisha alama 10 kileleni mwa kundi D ambapo imeipita Monastr kwa wastani wa magoli ya kushinda na kufungwa huku Real Bamako ikiwa katika nafasi ya tatu baada ya kuifunga 2-1 Tp Mazembe.

Yanga sc sasa itaifuata Tp Mazembe katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo huku Real Bamako ikikutana na Monastr katika funga dimba huku kila timu ikijitahidi kupata ushindi ili kupata kiasi kikubwa cha fedha huku kukwepa kupangiwa wababe wa makundi mengine katika raundi ya robo fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala