Klabu ya Yanga sc imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ikiwa ni raundi ya 16 mchezo wa kwanza wa duru la pili la ligi kuu nchini.
Yanga sc ilikumbana na upinzani mkali kutoka kwa Kagera sugar katika dakika za mwanzo wa mchezo hivyo kuwalazimu kusubiri mpaka dakika ya 30 ambapo uzembe wa kipa Ramadhani Chalamanda kuokoa krosi ya Saido Ntibanzokiza na mpira kumkuta Fiston Mayele ambaye alipiga kichwa na kufunga akiandika bao la kwanza ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Iliwachukua Yanga sc dakika tano za Kipindi cha pili kuandika bao la pili ikiwa ni krosi ya faulo ya Ntibanzokiza kuunganishwa na kichwa kikali cha Mayele na kumshinda Chalamanda licha ya juhudi za kutaka kuokoa hatari hiyo.
Saido alifaidika na kukaa katika eneo zuri na kupokea pasi mpenyezo ya Mayele na kuandika bao la tatu kwa Yanga sc ikiwa ni dakika ya 54 na mpaka mchezo unamalizika matokeo yalibaki kama yalivyo.
Yanga sc imejikita kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 42 na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi huku Kagera Sugar ikiwa katika nafasi ya nane na alama 20 katika michezo 16 ya ligi kuu.
“Tulitengeneza nafasi kwenye mchezo wetu na ilikuwa ni mchezo mzuri ila mwisho wa siku tumepoteza hivyo tunajipanga kwa ajili ya mechi zijazo,”.Alisema kocha Francis Baraza wa Kagera Sugar baada ya mchezo.