Connect with us

Makala

Yanga sc Yaisurubu Geita Gold Fc

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold Fc katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba siku ya Jumamosi Oktoba.

Yanga sc ikianza na kikosi kile kile cha mastaa wa siku zote wakiwemo Djigui Diarra,Yao Yao,Joyce Lomalisa,Dickson Job na Bakari Mwamnyeto huku eneo la kiungo likiwa na Mudathir Yahaya,Khalid Aucho,Pacome Zouzou,Aziz Ki,Max Nzengeli huku Clement Mzize akiongoza eneo la ushambuliaji.

Iliwalazimu Yanga sc kusubiri mpaka dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza kupata bao la dakika ya 44 kupitia kwa Pacome aliyeunganisha mpira wa pasi kutoka kwa Yao Yao huku dakika moja baadae Aziz Ki aliipatia Yanga sc bao la pili akiunganisha pasi ya Max Nzengeli.

Geita Gold Fc kipindi cha pili walijitahidi kufunguka na kuacha kupaki basii huku uimara wa beki Kelvin Yondani na Onditi katika eneo la kiungo kuliwapa nafuu ya kutofungwa na Yanga sc mabao mengi.

Max Nzengeli aliwapatia Yanga sc bao la tatu baada ya Mudhathir Yahaya kumnyan’ganya mpira kiungo wa Geita dakika ya 69 ya mchezo ambapo mpaka mpira unamalizika matokeo yalibaki kuwa 3-0.

Geita Gold Fc sasa haina budi kuongeza bidii ili kujikwamua kutoka mkiani ikiwa katika nafasi ya 12 ya msimamo ikiwa na alama 4 katika michezo mitano ya ligi kuu nafasi ambayo sio nzuri huku Yanga sc ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo ikiwa na alama 12.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala