Connect with us

Makala

Yanga sc Yaipiga Prisons 4

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kufuzu raundi inayofuatia ya michuano ya kombe la shirikisho nchini Tanzania baada ya kuifunga Tanzania Prisons kwa mabao 4-1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki hasa wa Yanga sc.

Wenyeji wakiwapumzisha baadhi ya mastaa kama Fiston Mayele,Dickson Job,Khalid Aucho na Yannick Bangala walianza kuandika bao la kwanza likifungwa na nahidha Bakari Mwamnyeto dakika ya 52 ambapo Dakika nane baadae Jumanne Elfadhil aliswazisha kwa kichwa lakini mabao mawili ya kinda Clement Mzize dakika za 70 na 88 huku Stephane Aziz Ki akifunga pia kwa penati dakika ya 85 yalitosha kuwafungia virago wajelajela hao.

Yanga sc baada ya kuibuka na ushindi huo imefuzu katika hatua ya nusu fainali ikiunga na timu za Simba sc,Singida Big Stars huku zikisubiriwa mechi kadhaa ili kujua hatua ya robo fainali itakuaje.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala